ALICHO ONGEA WYNE ROONEY BAADA YA KUSIKIA NDUGU YAKE KAPANDA MLIMA KILIMANJARO - The Choice

ALICHO ONGEA WYNE ROONEY BAADA YA KUSIKIA NDUGU YAKE KAPANDA MLIMA KILIMANJARO

0

August 18 2016 ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa Anthony McLoughlin ambaye ni shemeji wa mshambuliaji wa kimataifa wa England anayeichezea Man United Wayne Rooney, Anthony August 18 alifanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro uliopo Tanzania.

Anthony amepanda mlima Kilimanjaro ikiwa kama ni sehemu ya kumkumbuka mdogo wake Rosie aliyefariki akiwa na umri wa miaka 14 kutokana na matatizo ya rare genetics disorder (Rett Syndrome) na kuchangisha fedha kwa ajili ya Claire House Charity ambao walikuwa na mchango mkubwa kwa Rosie.

Wayne Rooney

Wayne Rooney

Siku nane baada ya Anthony kupanda mlima Kilimanjaro  na kufika kileleni, Wayne Rooney ambaye ni shemeji yake na Anthony alitumia ukurasa wake wa twitter kumpongeza Anthony, kama hufahamu Anthony ni kaka wa mke wa Wayne Rooney ambaye anajulikana kwa jina la Coleen Rooney.

Facebook Comments
Share.

About Author