Alichokisema Bocco wa Azam Fc Baada ya Kuwafunga - The Choice

Alichokisema Bocco wa Azam Fc Baada ya Kuwafunga

0
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amesema kwamba utulivu, kutokata tamaa ndiyo siri ya mafanikio yake kuifunga mara nyingi Simba kila wanapokutana nayo.
Bocco alifunga bao pekee la dakika ya 70 jana kwa Azam kwenye mchezo dhidi ya Simba iliyolala kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza  baada ya mchezo wa juzi, Bocco alisema kwamba kufunga kwake kwenye mechi nyingi dhidi ya Simba kunatokana na utulivu na kutokata tamaa muda wote wa mchezo.
“Kila mechi nawekewa ulinzi mkali, lakini sikati tamaa, muda wote ninakuwa na lengo moja tu la kutafuta nafasi ya kufunga, ambalo ndilo jukumu langu nililopewa uwanjani kama mshambuliaji,”alisema Bocco na kuongeza.
“Mfano mechi kama ya leo (juzi) mimi ninapenda niwasifu mabeki wa Simba walicheza vizuri na kutubana kwa muda mrefu, lakini likatokea kosa moja tu na sisi tukalitumia vizuri kujipatia bao,”alisema Bocco.
Bao la juzi linakuwa la nane kwa Bocco msimu huu na kuzidiwa kwa bao moja na Shiza Kichuya wa Simba, Amissi Tambwe na Simon Msuva wa Yanga wanaoongoza kwa pamoja kila mmoja akiwa na mabao tisa.
Aidha, juzi Bocco aliifikisha mabao 19 ya kuifunga Simba tangu Azam ipande Ligi Kuu mwaka 2008, hivyo kuendelea kuongoza kufunga mabao mengi katika mechi baina ya timu hizo.
Share.

About Author