Home Michezo Alichosema Masau Bwire baada ya Kufungwa na Yanga,Awaita Yanga jina Hili..

Alichosema Masau Bwire baada ya Kufungwa na Yanga,Awaita Yanga jina Hili..

210
0

 

Masau Bwire msemaji wa Ruvu Shooting kama kawaida yake baada ya mchezo wa raundi ya 14 kati ya Ruvu waliokuwa wenyeji wa Yanga uwanja wa Uhuru amesema Waamuzi wa Mchezo kati Yao na Yanga waliwaumiza Ruvu Shooting na Kuibeba Yanga.

Masau ambaye huwa anamaneno anaposhinda na hata anaposhindwa amesema Mwamuzi wa Mchezo wa Leo amewanyima penati na Kuna Matukio mengine karibu saba ambayo yamewanyima Ushindi Ruvu Shooting .

” Kweli tumefungwa goli moja halali kabisa lakini waamuzi wa Leo walichofanya ilikuwa nimkudhoofisha Ruvu Shooting angalia penati ile ilikuwa na tatizo gani? Nafikiri bodi ya ligi iwatazame waamuzi wa Leo kama ilivyokuwa ikiwafungia wanaovurunda Basi na Hawa iwaangalie na kuwachukulia hatua ”

Alimaliza Masau Bwire.

Masau Pia  amesema Yanga ni wazee na katika mchezo wa Jana Basi walikuwa wamechoka wakicheza na vijana wake sema wajukuu (marefa ) wamewaokoa kutoka kwenye kipigo cha Ruvu Shooting.

” Kama ukiangalia mpira wa Yanga aisee wamechoka ni wazee Hawa sema wajukuu wa jadi wamewasaidia kutopata kipigo ”

Yanga katika mchezo huo walifanikiwa kupata Ushindi wa bao moja kwa bila bao likipatikana kipindi cha Kwanza katika dakika 5 ya nyongeza goli likifungwa na Pius Buswita aliyesajiliwa kutoka Mbao Fc ya Mwanza kwa kichwa akipokea krosi safi ya Mchezaji Ibrahim Ajib aliyekuwa Winga ya Kulia goli lililodumu mpaka mpira unamalizika

Leave a comment