Home News APE NETWORK YAJIPANGA KUSAMBAZA KISWAHILI DUNIANI KUPITIA MICHEZO YA JUKWAANI

APE NETWORK YAJIPANGA KUSAMBAZA KISWAHILI DUNIANI KUPITIA MICHEZO YA JUKWAANI

2019
0

Abraham Ntambara

KAMPUNI ya Africa Proper Education Network (APE Network) imejipanga kusambazi Lugha ya Kiswahili Afrika na Dunian kote kupitia michezo ya jukwaani.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa APE Network Hermes Damian akizngumza kwenye Onesho la Bibi Titi Mohamed.

Hayo yalisema jana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa APE Network Hermes Damian alipokuwa akizungumza kwenye Onesho la Tamthilia ya  Bibi Titi Mohamed liloonyeshwa na Kaleleo Sanaa Network ikiwa ni sehemu ya usahili wa tamthilia hiyo inayotarajiwa kuonyeshwa Oktoba 26, 2018 katika Tasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

“APE Network inatambua kuwa Lugha ya Kiswahili ni tunu adhimu inayotuwezesha wapenzi wote wa lugha ya Kiswahili kuwasiliana na kutupa utambulisho kote duniani. Kutokana na hili, Kiswahili ni zana inayotuwezesha sisi kama taifa kueneza sanaa, tamaduni na historia yetu Duniani kote,” alisema Damian.

Alisema kutokana na umuhimu huo kampuni hiyo kwa kuptia kitengo chake cha uhifadhi na uenezaji wa Kiswahili na Jukwaa la Kiswahili  imeamua kuanza kufadhili kazi mbali mbali za sanaa ikiwa ni pamoja na Tamthilia hiyo ya Bibi Titi Mohamed iliyochezwa na Kaleleo Sanaa Network.

Damian alibainisha kuwa kuimarika kwa nafasi ya Kiswahili Duniani kunatoa fursa kwa waandishi, wachapishaji, wasanii na Taifa kwa ujumla kusambaza kazi na maarifa kwa watu wengi zaidi ulimwenguni sambamba na kutangaza umahiri wa wanazuoni na watalaam wetu.

“Jukwa la Kishahili limeandaa mpango kazi wa kunadi Kiswahili na Utamaduni wetu sambamba na kunyanyua utamaduni wa kuangalia maigizo jukwaani kwa kupitia kazi mahiri za waandishi wetu,” alisema.

Mkurugenzi wa Kaleleo Sanaa Network na Mwangozaji wa Tamthilia ya Malkia Bibi Titi Mohamed Ghonche Materego akizungumza kwenye Onesho la Bibi Titi Mohamed.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kikundi cha Kaleleo Sanaa Network ambaye pia ni mwongozaji wa Tamthilia ya Malkia Bibi Titi Mohamed Ghonche Materego, alisema lengo la kikundi ni kuendeleza kazi za sanaa na vipaji vya wasanii kupitia uandaaji wa maonyesho ja jukwaani.

Akizungumzia lengo la Tamthilia ya Bibi Titi, alisema ni kutaka kuonyesha historia ya mwana mama mwanaharakati ushiriki wake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa mkoloni.

“Vizazi vya leo vinaweza vikakosa historia yake na visijue waliohusika kutafuta uhuru, tunachuhimiza katika tamthilia hii ni akina mama na wasichana wasijisikie wanyonge kutetea maslahi katika jamii,” alisema.

Mtunzi wa Tamthilia ya Malkia Bibi Titi Mohamed na Mwandishi wa Vitabu Profesa Emmanual Mbogo akizungumza wakati wa Onesho.

Kwa upande wake mtunzi wa tamthilia hiyo na mwandishi wa vitabu Profesa Emmanuel Mbogo alisema tamthilia hiyo inaonyesha histolia ya tulipotoka, changamoto walizokutana nazo wapigania uhuru, lakini pia jinsi mwanamke kama Bibi Titi Mohamed alivyoshiriki katika kumuondoa mkoloni.

Hivyo Profesa Mbogo alieleza kuwa kwa kielelezo cha mwanaharakati mwana mama inaonyesha ni jinsi gani mwanamke akipewa nafasi katika jamii anaweza kutoa mchango wake katika maendeleo na hii mi kutokana na kwamba mwanamke amekuwa akidharauliwa na kutopewa nafasi ya kutoa mchango wake.

Jukwaa la Kiswahili ni shirikisho/ jumuiko la waandishi na wanazuoni wa Kiswahili lenye lengo la kukusanya, kuendeleza , kuhifadhi na kusambaza kazi za kiswahili ili kutoa elimu na kueneza utamaduni wa Mswahili na Mtanzania ulimwenguni kote. Jukwaa la kiswahili limeanzishwa na Kampuni ya APE Network.

Kikundi cha Kaleleo Sanaa Network kikifanya Onesho la Bibi Titi Mohamed.