ARSENE WENGER: SINA MPANGO WA KUONDOKA ARSENAL

0

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameendelea kusistiza kuendelea kufanya kazi klabuni hapo kwa msimu ujao, licha ya mkataba wake kutarajiwa kufikia kikomo mwezi Julai.

Wenger amezungumza na waandishi wa habari mchana huu na kuwaeleza suala hilo, kufuatia tetesi zinazomuandana kuhusu uwezekano wa kuwa miongoni mwa watakaowania nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi la FC Barcelona

Wenger amsema hana mpango wa kuelekea nchini Hispania kufanya kazi ya ukufunzi, na hata kama itatokea viongozi wa FC Barcelona wataonyesha nia ya dhati ya kutaka kufanya nae kazi, bado itakua vigumu kwake kufanya maamuzi.

amesema: “Mipango yangu ni kutaka kuendelea kuwa meneja wa Arsenal, lakini suala hilo litaamuliwa na viongozi wa juu, kutokana na mkataba wangu kuwa mbioni kufikia kikomo.

“Klabu inaweza kufanya maamuzi yoyote, lakini bado ninatamani kuendelea kubaki hapa na kufanya kazi. Sitafuti kazi sehemu nyingine yoyote.”

Facebook Comments
Share.

About Author