Home News AWESO NA KAMPENI YA “MRADI KWA MRADI” YAMFIKISHA KIJIJI AMBACHO WAKAZI WAKE...

AWESO NA KAMPENI YA “MRADI KWA MRADI” YAMFIKISHA KIJIJI AMBACHO WAKAZI WAKE HAWAJAWAHI KUULIZA SWALI KWA WAZIRI MOJA KWA MOJA

1458
0
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akitazama gari lake “lilivyokula vumbi” wakatika wa ziara ya “mradi kwa mradi” kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inawafikia wananchi kwa uhakika huko wilayani Wanasimanjiro.

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akishiriki kunasua gari la polisi lililokwama kutokana na matope yaliyosababishwa na mvua wakati akiwa katika ziarab hiyo

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), akipokewa na kina mama wa Kata ya Olchorinyori, wilayani Simanjiro , mkoa wa Manyara alipoenda kufuatilia ujenzi wa miradi ya maji, ikiwa ni sehemu ya ziara ya mradi kwa mradi mkoani Manyara.

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikaribishwa Kata ya Olchorinyori, Simanjiro  baada ya kuvishwa vazi la kitamaduni la kabila la Maasai.

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)  akiongea na wanakijiji wa kata ya Olchorinyori, Simanjiro . Waziri Aweso (Mb) ameelekeza wanakijiji hao wachimbiwe kisima cha maji karibu na makazi yao ili waweze kutumia kwa matumizi ya nyumbani na kuhudumia mifugo, wakati wakisubiri mradi mwingine wa maji, pia kuzuia kupeleka mifugo katika vyanzo vya maji.

 

Mkazi wa Kijiji cha Olchorinyori, wilayani Simanjiro Bw. Nganeni Mirerei akiuliza swali wakati wa kikao kuhusu miradi ya maji kilichowakutanisha baadhi ya wanakijiji wa Kata ya Olchoronyori na Waziri Aweso.

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikagua mradi wa maji wa Mirerani ambapo ametoa siku tano za kazi,kuanzia tarehe 26.10.2018 kwa Wakala ya Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) kufanya majaribio ya pampu ili kazi nyingine zifanyikewa. Hali ya upatikanaji majisafi na salama wilayani Simanjiro ni wastani wa asilimia 42 ambayo inatakiwa kuongezeka.

 

Mkutano ukiendelea katika eneo la mradi wa maji wa Olbil – Simanjiro ambao miundombinu ya maji imewekwa kwa thamani ya shilingi milioni 312. Waziri Aweso amewataka watalaam wa maji kuhakikisha chanzo cha maji cha uhakika kinapatikana kwanza kabla ya hatua nyingine ikiwamo uwekaji miundombinu ya maji katika mradi wowote wa maji hapa nchini 

 

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwasikiliza wananchi wilayani Simanjiro waliolalamika mkandarasi kampuni ya Meero Ltd aliyepewa kandarasi ya mradi wa maji wa Orbil kulaza mabomba kwa kina kidogo (kama inavyoonekana pichani). Mkandarasi kaelekezwa kurekebisha kasoro hiyo kwa gharama zake mwenyewe ambapo ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni 312.3.

 

  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiendesha kikao katika makazi ya wanakijiji jirani na mradi wa maji wa Orbil, ambao wanakijiji wanategemea kunufaika nao mara utakapokamilika kwa kuwa na uwezo wa kuhudmia wananchi wapatao 7, 500.

 

 

 

 

Baadhi ya wakazi wa kata ya Olchorinyori wakifurahia mae;lezo ya Mhe. Awesso waliposhiriki kikao kwa mara ya kwanza kijijini kwao na Waziri.

 

Wakazi wa Kata ya Olchorinyori wakifurahi, pamoja na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) baada ya kumaliza kikao, kijijini Olchorinyori-Simanjiro.