Azam yamuuza Tchetche Oman - The Choice

Azam yamuuza Tchetche Oman

0

MATAJIRI wa Ligi Kuu Bara, Azam wanatarajia kuingia msimu mpya wakiwa wamegusa; benchi la ufundi na safu ya ushambuliaji na tayari imetangaza kuachana na Kipre Tchetche aliyejificha jijini Dar es Salaam.

Azam imefanya mabadiliko makubwa katika benchi la ufundi, imeleta makocha Wahispaniola; Kocha Mkuu Zeben Hernandez,  msaidizi Yeray Romero, kocha wa viungo, Jonas Garcia na wa makipa, Pablo Borges.

Makamu Mwenyekiti Azam, Nassoro Idrissa ‘Father’ alisema: “Nadhani mabadiliko makubwa yapo benchi la ufundi na  safu ya ushambuliaji, tunatafuta mbadala wa Allan Wanga na Kipre Tchetche, nafasi za wachezaji wa kigeni zipo nne; Wanga, Racine Diouf na Kavumbagu waliondoka, Kipre tupo hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kwenda Oman,” alisema.

Azam ina nyota wanne wageniwanaofanya majaribio kutoka Niger,  Zimbabwe na Ivory Coast.

Facebook Comments
Share.

About Author