“Bila Arsenal nisingefika hapa” – Fabregas. - The Choice

“Bila Arsenal nisingefika hapa” – Fabregas.

0

 

Mwaka 2011 kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Hispania Cesc Fabregas aliondoka Arsenal na kwenda kujiunga na timu yake ya nyumbani ya Barcelona.Usajili huo uliwauma mashabiki wengi wa Arsenal lakini mwaka 2014 Arsenal waliumia zaidi.Arsenal waliumia baada ya Cesc kujiunga na wapinzani wao timu ya Chelsea.

Kuanzia hapo mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimpa wakati mgumu sana Fabregas pale timu hizo mbili zinapokutana.Wamekuwa wakimzomea sana na kauli ya Fabregas ya kusema amefuata makombe katika timu ya Chelsea.Kauli hiyo ilionekana kama kutonesha kidonda kibichi kwa Arsenal kwani walikuwa hawajabeba makombe kwa muda mrefu.
Wikiendi hii Fabregas anakutana tena na timu yake ya zamani.Lakini safari hii Fabregas ameyakumbuka maisha ya Emirates.Fabregas anasema “sijali kuhusu mashabiki wanawaza nini kuhusu mimi lakini najali nini nawaza kuhusu wao,kuna mambo mengi hayawezi kubadilika,mengi yamesemwa kuhusu mimi,kila kona nimekuwa nikiongelewa.”
“Arsenal ni sehemu bora sana kwangu,ndio timu ambayo iliniamini,nilikuwa kijana mdogo wa miaka 16 na wao ndio walinila nafasi katika timu yao,Arsene Wenger na timu kwa ujumla walinipa nafasi katika timu”.aliongeza Fabregas.Akiwa na miaka 21 tu kocha Wenger aliamua kuonesha imani yake kwa Fabregas kwa kuamua kumpa beji ya ukapteni.
Fabregas anaishukuru sana timu ya Arsenal na haamini bila Arsenal angeweza kufika alipo “Arsenl ndio walinifanya niitwe timu ya taifa nikashinda kombe la dunia na kombe la Ulaya,hakika lazima niwe na shukurani kubwa kwa klabu hii” alimalizia Cesc.
Share.

About Author