BREAKING NEWS:HANS POPPE AJIUZULU SIMBA KISA SPORT PESA

0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili SimbaZacharia Hans Poppe ameachia ngazi.
Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi baada ya kuona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo katika klabu hiyo.

“Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo na kuongeza:
“Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka automatically katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati hiyo.
“Kilichomchukiza ni kwamba kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimyakimya na Hans Poppe amesema hata Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo
Facebook Comments
Share.

About Author