BREAKING NEWZ YANGA YAMFUTA KAZI MKURUGENZI WA UFUNDI, HANS VAN PLUIJM

0
Kufuati hali ugumu ya kiuchumi inayoikabili klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imemfuta kazi Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo Hans Van Pluijm.
Katika barua aliyokabidhiwa jana, Yanga walieleza sababu ya kuvunja mkataba na raia wa Uholanzi kuwa ni matatizo ya kifedha.
“Nimepewa barua asubuhi hii (jana) na Yanga juu ya mkataba wangu kuwa umesitishwa, kikubwa walichokisema ni kuwa klabu kwa sasa inakabiliwa na ukata hivyo hawana uwezo wa kuendelea kunilipa.”
“Kwa sasa nipo huru kujiunga na klabu yeyote itakayoonyesha nia na mimi basi nitafanya nao kazi” alinukuliwa Hans Van Pluijm.
Pluijm alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga huku nafasi yake kama kocha mkuu wa Yanga ikichukuliwa na raia wa Zambia, George Lwandamina.
Wakati huo huo, Obrey Chirwa amefutiwa kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting, sasa yupo huru kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa kesho utakaopigwa huko Morogoro.
Katika mchezo uliopita Mzunguko wa kwanza dhidi ya Mtibwa , Chirwa alipachika kimiani magoli 2 katika ushindi wa magoli 3 -1 walioupata Yanga SC.
Facebook Comments
Share.

About Author