Home Michezo CHRISTIANORonaldo huenda akajiunga na timu hizi

CHRISTIANORonaldo huenda akajiunga na timu hizi

17
0


Baada ya kuipa mafanikio makubwa klabu yake ya Real Madrid ya Spain, Cristiano Ronaldo ameutaarifu uongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka.

Gazeti la A Bola la Ureno limeripoti na kuzihusisha klabu za PSG na Manchester United kuwa ni timu ambazo huenda akajiunga nazo.

Hatua hii ya Ronaldo ambaye pia ni mshindi mara nne wa tuzo ya ‘Ballon d’or’ inakuja baada ya kupata kesi ya ukwepaji kodi.

Katika hatua nyingine gazeti la Marca limeripoti tetesi kuwa Real Madrid imeiambia Man United iandae Pauni 160 milioni, kama inamtaka mkali huyo.