Daktari afunguka kama Kamusoko atakuwa fiti mechi ya Azam Au atakosekana

0

Daktari afunguka kama Kamusoko atakuwa fiti mechi ya Azam Au atakosekana

Jumamosi katika uwanja wa Azam Fc (Azam Complex) kutakuwa na Darby ya Dar Es Salaam Azam Fc dhidi ya Yanga moja kati ya Mchezo ambao wapenzi wa soka nchini wanausubiri kwa hamu Kubwa kutokana na upinzani uliopo baina yao kila mara wanapokutana.

Kuelekea pambano hilo Daktari wa timu ya Yanga Edward Bavu amesema kuwa Kamusoko itakuwa ngumu kucheza mchezo unaofuata dhidi ya Azam Fc siku ya Jumamosi.

” Ni kweli kamusoko ameanza mazoezi kidogo kidogo lakini kwenye kikosi cha jumamosi bado hatakuwa na nafasi, kwa mchezaji ambaye amekuwa majeruhi kwa muda mrefu kuna aina ya mazoezi anatakiwa kuyafanya, tunashukuru ameanza kukaa sawa lakini kwa mchezo ujao bado hatakuwepo. “

SHAIBU NINJA TAA YA KIJANI MECHI NA AZAM

Beki wa kati wa timu ya Yanga Abdallah Shaibu aliyeumia kwenye mashindano ya Mapinduzi yeye amerejea katika mazoezi na kama kocha ataona anafaa kutumika katika mchezo ujao basi yuko fiti baada ya Kupona Bavu ameithibitishia Kwataunit.com

Yanga imekuwa inakumbwa na Majeruhi mara kwa mara huku baadhi ya wachezaji wakiwa ni majeruhi wa Muda Mrefu lakini taraibu wameanza kuwa Fiti.

Upande Mwingine Yanga wameendelea kufanya mazoezi wakitokea Kambini ambapo wameweka kambi kujiwinda na mchezo dhidi ya Azam Jumamosi

1,231 total views, 6 views today

Facebook Comments
Share.

About Author