Dili limekamilika: Jose Mourinho kusaini mkataba Manchester United ndani ya masaa machache - The Choice

Dili limekamilika: Jose Mourinho kusaini mkataba Manchester United ndani ya masaa machache

0

jose-mourinho_10ql0j6pkluu81sts81jdf12mk

Jose Mourinho anakaribia kutangazwa kuwa meneja mpya wa Manchester United kwa mujibu wa habari

Mkongwe huyo wa miaka 53 amehusishwa sana na tetesi za kutua Old Trafford tangu alipotimuliwa Chelsea Desemba mwaka jana.

Bosi wa sasa Louis van Gaal amewekwa kitimoto baada ya kushindwa kufanya vizuri katika kampeni za msimu huu, jambo ambalo limeifanya Manchester United ishindwe kutamba katika mbio za kuwania taji Ligi ya Uingereza.

United kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, pointi mbili nyuma ya Manchester City inayoshika nafasi ya nne, na ni wazi kwamba wameshindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo watacheza dhidi ya Crystal Palace katika fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley baadaye mwezi huu.

Lakini inaonekana hata kama wakitwaa kombe la FA, bado mafanikio hayo hayatatosha kuokoa kibarua cha Mdachi huyo.

Iliripotiwa kuwa Mourinho alisaini mkataba wa awali Februari, kabla ya Ed Woodward kusita kumtimua van Gaal.

Mkurugenzi wa Old Trafford alimtaka sana bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino kama mrithi sahihi wa Louis van Gaal.

Lakini inaonekana sasa Mourinho anatimiza ndoto yake, kuinoa Manchester United.

The Special One kwa sasa yupo Mexico akiinoa timu ya malegendari wa FIFA

Facebook Comments
Share.

About Author