Home Michezo DK MWAKYEMBE AMKINGIA KIFUA SAMATTA, HIKI HAPA AMESEMA

DK MWAKYEMBE AMKINGIA KIFUA SAMATTA, HIKI HAPA AMESEMA

1482
0

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harisson Mwakyembe amemkingia kifua nahodha wa timu ya Taifa Mbwana Samatta kwa kukosa penati kwakuwa ni sehemu ya mchezo ila hajaridhika na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

Mwakyembe alisema kuwa kwa ushindi huo wamerejesha imani kwa watanzania pamoja na furaha licha ya kukosa nafasi ambazo walizitengeneza ndani ya uwanja .

“Achana na suala la kukosa penati,hiyo ni sehemu ya mchezo ila wameonyesha namna ambavyo thamani ya bendera ya taifa inakuwa hasa kwa kupata ushindi¬† katika uwanja wa nyumbani.

“Tulipaswa tufunge mabao mengi mpaka matano ila yote ni matokeo , bado tuna nafasi ya kuweza kusonga mbele wachezaji wanatakiwa waendelee kuonyesha juhudi¬† watanzania wanawafuatilia ,lengo ni kuweza kufuzu.”alisema.