Home News DK. SHIKA KUJENGA KIWANDA CHA TAULO ZA WANAWAKE KILIMANJARO

DK. SHIKA KUJENGA KIWANDA CHA TAULO ZA WANAWAKE KILIMANJARO

2247
0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Kampuni ya Ralcefort ya nchini Urusi Dk. Luis Shika amesema kuwa anatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza TV za kike mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Dk. Shika alibainisha kuwa kujengwa kwa kiwanda hicho ni zawadi kwa wanawake kuelekea sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya na taulo hizo zitakuwa zikitawanywa bure.

“Zawadi hii naitoa kama zawadi ya Krismasi hii na mwaka mpya unaoingia wa 2019, natoa zawadi ya kiwanda cha kutengeneza taulo za kike bure, kiwanda hiki kitatengeneza taulo hizi na kuzitawanywa bure kwa wahitaji wote Duniani,” alisema Dk. Shika.

Aliomba viongozi wa mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro kumwandalia eneo ambalo atajenga kiwanda hicho na kueleza kuwa kiwanda hicho kitasimamiwa na Julieth Maleko na Konfesta.

Dk. Shika alisema kiwanda hicho kitajengwa na Wajapani hivyo anachosubiri ni wao kufanya usanifu wa ujenzi na kupewa gharama kwa ajili ya malipo kwani fedha ipo.

Akitoa sababu ya kuwapa wajapani kujenga kiwanda hicho alisema ni kutokana na kwamba baadhi ya fedha zake zipo nchini Japani hivyo itakuwa rahisi kuwalipa.

Katika hatua nyingine Dk. Shika alisema yupo katika mchakato wa kuisajili kampuni yake nchini na kwamba kabla ya kufanya usajili huo kati ya Disemba 27 na 28 anatarajia kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji wilayani Kigambni.

“Ninatoa misada ya bure kwa walengwa wachache, sina uwezo wa kuwapa msaada watanzania wote wenye uhitaji lakini watakao kuwa na bahati ndiyo hao hao, misaada hii itatolewa Kigamboni katika eneo linaloitwa Tungi,” alisema Dk. Shika.

Alisema misaada hiyo ataitoa akiambatana na viongozi wa Urusi na kubainisha makundi yatakayopatiwa msaada huo kuwa ni wajane, mayatima na wafanyabiashara wadodgo wadogo.