Home Burudani FILAMU ALIYOSHIRIKISHWA RAY ‘IMETOSHA’ KUONEKANA KIMATAIFA KUPITIA APP YA MPtv

FILAMU ALIYOSHIRIKISHWA RAY ‘IMETOSHA’ KUONEKANA KIMATAIFA KUPITIA APP YA MPtv

1471
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
FILAMU mpya inayokwenda kwa jina la ‘IMETOSHA’ mbayo ameshirikishwa msanii wa Filamu za kibongo maarufu kama ‘Bongo Movie’Vincent Kigosi ‘Ray’ kuanzia mwezi ujao itakuwa ikionekana kimataifa kupitia APP ya MPtv.
Katikati ni Msanii wa Filamu nchini Vincent Kigosi maarufu ‘Ray’ akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar s Salaam.

 

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Ray alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya filamu hiyo kuanza kuoneshwa kupitia MPtv, alisema filamu hiyo ni nzuri na kuwaomba watanzania kuwaunga mkono kwa kuitazama.
“Leo nipo hapa kutangaza rasmi filamu hii itakuwa ikipatikana kupitia MPtv, filamu hii nimeshirikishwa na imeshutiwa nchini Zambia, na katika hiyo sinema kuna wasanii kama Kajala Masanja na Cassie Kabwita,” alisema Ray.
Katika filamu hiyo Ray alibainisha kuwa ameshiriki kama msanii wa kimataifa na kubainisha kwamba ni filamu ambayo inakuja kuleta mabadiliko makubwa kwenye tasnia ya filamu nchini.
Katikati┬áni Ofisa Mipango wa MPtv Nchini Daudi Michael ‘Duma’ akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Aidha Ray alisema ujuo wa MPtv nchini ni mkombozi kwa wasanii wa filamu nchini kwani licha ya kupata fedha msanii anaingia nao makubaliano ya muda fulani na hawachukui hati miliki hivyo baada ya muda wa makubaliano kwisha unaruhusiwa kuitumia kwa matumizi yako binafsi kwa kadri ya mapenzi yako.
Katika hatua nyingine Kulwa Kikumbe maarufu kama ‘Dude’ ambaye pia ni msanii wa filamu nchini ametangaza pia kuanzia mwezi ujao filamu yake ya ‘Bongo Dar es Salaam’itakuwa ikionekana kupitia MPtv.
“Nimekuwa nikiulizwa saana juu ya filamu yangu ya Bongo Dar es Salaam, hivyo kuwanzia mwezi ujao mwendelezo wa filamu hii utakuwa ukipatikana katika App ya MPtv, tumekuwa tukilia saana kuibiwa kazi zetu, lakini kwa njia hii itakomesha wizi,” alisema Dude.
Kuanzia kulia ni Dude, Ray na JB walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Balozi wa MPtv nchini Jocob Stephen ‘JB’ alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wazalishaji wa filamu nchini kutangaza filamu zao ili zifahamike na hatimaye zinunuliwe kwa ajili ya kuzionesha kupitia APP hiyo.
Naye Afisa Mipango wa MPtv nchini Daudi Michael ‘Duma’ alisema kutangazwa kwa filamu hizo ni mwendeleo wa APP hiyo kwa kila mwezi kutangaza filamu mpya ambazo zitakuwa zimenunuliwa kwa ajili ya kuoneshwa kupitia TV hiyo.