Goli la John Bocco Laua Shabiki wa Simba Dar - The Choice

Goli la John Bocco Laua Shabiki wa Simba Dar

0
BAO la dakika ya 70 alilofunga straika wa Azam FC, John Bocco, juzi Jumamosi dhidi ya Simba, limeua shabiki mmoja wa Simba aliyetajwa kwa jina la Chenje Ramadhan Dogoli mkazi wa Manzese jijini Dar, mwenye umri wa miaka 39.
Kwa mujibu wa nesi wa Hospitali ya Mwananyamala ambaye hakupenda kuanikwa jina lake kwa sababu yeye si msemaji mkuu, alisema shabiki huyo ambaye ni mfanyabiashara katika eneo la Manzese, alifikishwa hospitalini hapo na wenzake akiwa kwenye hali mbaya.
“Alifikishwa hapa na wenzake akiwa kwenye hali mbaya, wenzake wanasema
 wakati wanaangalia mpira huko kwao Manzese, mara bao lilipofungwa, akaonekana anapumua kwa taabu na akaanza kuishiwa nguvu, wakaamua kumkimbiza hospitali ambapo kwa bahati mbaya akafariki dunia muda mfupi baada ya kufika hapa,” alisema nesi huyo ambaye ndiye aliyempokea.
Ikumbukwe kuwa, Simba na Azam zilipambana juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na Azam kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Bocco ukiwa
 ni mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Bara.
Hata hivyo, walipotafutwa madaktari wa Mwananyamala jana, waligoma kuzungumzia ishu hiyo wakidai wafuatwe ofisini leo Jumatatu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Suzan Kaganda alipoulizwa alisema suala hilo haliihusu polisi.
“Ishu hizo kama za kufa pengine kwa shinikizo la damu haziwezi kuripotiwa polisi kwa kuwa ni maradhi ya kawaida, labda ingekuwa ni jambo la mauaji,” alisema Kaganda.
Facebook Comments
Share.

About Author