Griezman azidi kufufua matumaini ya uhamisho wake kwenda United. - The Choice

Griezman azidi kufufua matumaini ya uhamisho wake kwenda United.

0

Antoine Griezman uhamisho wake kwenda umekuwa kama kizungumkuti na kila siku kunatokea habari mpya.Griezman ni kati ya wachezaji bora kabisa katika kizazi hiki cha soka jina lake likitokea mara mbili nyuma ya wachezaji wawili Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi hii ikiwa katika tuzo za Ballon D’or na zile za FIFA.

Inafahamika wazi kwamba United wako katika mpango wa kumuunganisha Guriezman na swahiba wake wa Kifaransa Paul Pogba.Usajili huu huenda ukavunja rekodi ya dunia ya usajili inayoshikiliwa na Paul Pogba.Katika siku zilizopita kulienea habari kwamba tayari makubaliano binafsi kati ya Griezman na United yamefikiwa.
Lakini mwanzoni mwa wiki hii Griezman aliwaweka mashabiki wa United katika hali ya sintofahamu baada ya kuongea kauli inayoonekana kama kuwakatisha tamaa.Griezman alieleza furaha aliyonayo kuwa mchezaji wa Athletico Madrid.Griezman alielezea hamu yake kushinda makombe na Athletico Madrid huku pia akisema ana hamu sana kuhamia katika uwanja mpya na timu yake hiyo.
Kauli hiyo ni kama ilioneaha ni kwa jinsi gani Griezman anahamu na kubakia Athletico.Lakini sasa ni kama vile Griezman ameikana kauli hiyo.Siku ya Jumanne Griezman tena alitoa kauli inayoonesha kutokuwa na uhakika wa kubakia Athletico Madrid baada ya kumalizika kwa msimu huu wa La Liga.
“Nani ajuaye jinsi msimu utakavyoisha?!kama ukiisha vibaya sina budi nijiulize maswali kuhusu hapa nilipo” alisema Griezman.Hadi sasa Athletico Madrid hawana uhakika wa kuchukua kombe lolote kwani walishatupwa nje ya kombe la mfalme,La Liga nako matumaini yao ni finyu huku Champions League wakiwa na bahati mbaya sana nayo na hii inaonenesha endapo watashindwa kweli kuchukua kombe hata moja baasi inaweza kuwa mwisho wa Griezman kuichezea Athletico Madrid.
“Lakini pia najiuliza wapi naweza kwenda,siwezi kwenda Madrid kutokana na timu niliyopo vivyo hivyo uhasama kati ya Barcelona na Madrid siwezi kwenda,ligi ya Ujerumani hainivutii kwa sasa na ya Ufaransa sio kwa kipindi hiki kuhusu Uingereza nako nina mashaka na hali ya hewa ya huko” alisema Griezman.
Lakini tayari mshauri wake ameshazungumzia kwamba uhamisho wa Griezman kwenda United una faida kwake kama mchezaji.Vile vile Griezman ameshawahi kukiri kwamba anavaa jezi namba 7 uwanjanj kwa kuwa alipokuwa kijana alikuwa akivutiwa zaidi na David Beckham.Jezi namba 7 United haivaliwi kwani mchezaji aliyekuwa akiivaa Memphis Depay ameondoka.
Share.

About Author