Home Michezo Habari Tano Kubwa Kutoka Yanga Leo 13.12.2017 Ikiwemo na Mustakabali Wa Ngoma...

Habari Tano Kubwa Kutoka Yanga Leo 13.12.2017 Ikiwemo na Mustakabali Wa Ngoma Yanga

41
0

Ngoma Aomba Msamaha Yanga.

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga,Donald Ngoma amekubali kuuomba radhi uongozi wa klabu ya hiyo na kuruhusiwa kujiunga na wenzake ambao wanaendelea na mazoezi katika uwanja wa uhuru kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania siku ya Jumamosi mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ngoma ambae alikuwa akituhumiwa na klabu hiyo kwa kosa la kuondoka klabu lni humo na kutimukia nchini kwao.

Tambwe Arejea Dimbani..

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anaekipiga kunako klabu ya Yanga, Amis Tambwe, hapo jana amerejea Dimbani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza goti tangu kuanza kwa msimu huu.

Tambwe amerejea ikiwa klabu yake inaklelekea katika michuano mbalimbali ikiwemo ya Kombe la FA na Kombe la Mapinduzi huku pia tukitarajia kushudia akiisaidia klabu yake kufanya vyema kimataifa katika michuano ya CAF Champions league.

Kurejea kwa Tambwe kutaioa afadhali safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo ambayo mpaka sasa inashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.

Ajibu, Raphael Daud Ramadhani Kavwili Na Gadiel Michael Kurejea Kikosini, Yondani Nje Wiki Mbili.

wachezaji Ibrahim Ajib, Raphael Daudi, Ramadhani Kabwili na Gadiel Michael wanatarajiwa kuungana na wenzao wakati wowote wiki hii baada Kilimanjaro Stars kuondoshwa kwenye michuano ya Chalenji nchini Kenya.

Yanga bado itaendelea kuwakosa wachezaji walio kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes ambayo imetinga nusu fainali ya michuano ya Chalenji na itaivaa Uganda Disemba 15.

Kelvin Yondani atakuwa nje kwa muda wa wiki mbili baada ya kuumia nchini Kenya huku Thabani Kamusoko akiwa bado anaendelea na matibabu ya jeraha la goti.

Mchakato wa Mabadiliko Kuanza Leo.

Kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga inatarajiwa kukutana leo kuandaa maandalizi ya mchakato wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Hatima Ya Yanga Kimataifa Kujulikana Leo.

Droo ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika inatatajiwa kufanyika leo jijini Cairo Misri na Yanga kama muwakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo ambayo ubingwa wake upo mikononi mwa Wydad Casablanca Ya Morocco.