Home Michezo HAJI MANARA ATAMANI NYOTA HUYU WA AZAM ATUE MSIMBAZI.

HAJI MANARA ATAMANI NYOTA HUYU WA AZAM ATUE MSIMBAZI.

57
0

Jana Jumapili March 11-2018, klabu ya  Azam FC, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Mbao Fc.

Mabao ya Azam FC yalufungwa kiustadi na wachezaji waliotokea benchi kipindi cha pili, akianza winga  machachari kikosini hapo Idd Kipagwile, dakika ya 63 akimalizia kwa kichwa krosi safi ya beki wa kushoto Bruce Kangwa.

Dakika tisa baadae mshambuliaji Bernard Arthur, aliyeingia dakika ya 61 kuchukua nafasi ya Shaaban Idd, aliipatia bao la pili Azam FC kwa jitihada binafsi akimalizia pasi safi ya juu ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kabisa hivi sasa.

Mbao ilijitutumua na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 89, lililofungwa na James Msuva, mdogo wake na staa wa Tanzania, Simon Msuva, anayesakata soka la kulipwa nchini Morocco hivi sasa.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Afisa Habari wa Simba Sc Haji Manara alimsifia mfungaji wa Bao la kwanza Idd Kipagwile kwa kiwango kizuri anachokionesha mchezaji huyo na kwenda mbali kwa kusema ingekuwa bora zaidi winga huyo akajongea Unyamani.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Manara aliandika “Iddi kipagwile najua bado nchi haijakuelewa..lakini wenye macho ya maili Mia tushakuelewa…natamani nikuone ukiwa nje ukisukuma gozi huko…au uje unyamani” alimaliza manara huku akimtag Idd Kipagwile mwenyewe, Yusufbakhresa, Vanmohamed na Azamfc.

Kwa matokeo hayo Azam Fc inapanda hadi nafasi ya pili kwa alama 44 ikiwa na jumla ya mchezo 22, nyuma ya Simba Sc yenye alama 46 kwa michezo 20, na mbele ya Yanga yenye alama 43 kwa michezo 20.