Home Michezo Haji Manara awajia juu Makocha wa Taifa Staa kwa kumuacha Mkude,huu ndo...

Haji Manara awajia juu Makocha wa Taifa Staa kwa kumuacha Mkude,huu ndo ujumbe alio uandika

276
0

Na George Mganga

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amehoji kuachwa kwa mchezaji na kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude, kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Kauli hiyo imekuja kuafuatia kiungo huyo wa Simba, kukosekana katika majina 23 ya wachezaji wa Taifa Stars walioitwa leo na Kocha Salum Mayanga, huku akisema ni kiungo bora nchini kwa sasa.

Haji amesema mpira unachezwa hadharani, kitendo cha mchezaji huyo kuachwa ni kumkosea heshima Mkude kuliko kuikosea heshima chupa.

“Unamuachaje Mkude? Mwisho wa Siku sisi ni Watanzania. Hata kama si makocha lakini soka huchezwa hadharani, najiuliza tena na tena kwa viungo tulionao ni kweli Jonas Mkude hastahili kuitwa kwenye timu hii? Kwa sasa hakuna ubishi Jonas ndio kiungo mkabaaji ‘holding midfielder’ bora nchini, ni kumkosea heshima kuliko chupa” ameandika Manara.