Home Michezo HAJI Manara Azidi Kuivurumishia Marungu TFF ya Malinzi..Leo Amedondosha Nondo Hizi Nzito...

HAJI Manara Azidi Kuivurumishia Marungu TFF ya Malinzi..Leo Amedondosha Nondo Hizi Nzito Huko Instagram..!!!

152
0

Mkuu wa  Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka mapya huku akidai yeye siyo mtu anayeamini uonevu na wala siyo mtu ambaye anaweza kunyamaza akiona haki yake inaporwa.

Manara amesema hayo kupitia ukurasa wa kijamii Istagram alfajiri ya kuamkia leo huku akilalama kuwa ‘Natural justice’ katika nchi hii haitambuliki kwa kuwa hakupatiwa nafasi ya kusikilizwa upande wake binafsi kabla ya kupewa hukumu.

“Natural justice nchi hii haitambuliki! wahaini na wauaji nao pia husikilizwa, iweje kwa mtuhumiwa ambaye anapigia kelele haki ya mwajiri wake?…..Ni aina ya hukumu katili zaidi kwa viwango vya mpira wetu ila nawaambia TFF Haji  Manara hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili lakini nina moyo wa simba nitapambana kwa kiwango cha juu sana”. Ameandika Manara

Vile vile Manara amesema atadai haki yake pamoja na mwajiri wake kwa viwango huku akiziomba kamati za Shirikisho za Soka Tanzania (TFF) zipokee rufaa yake .

“Nitaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa, nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki”. Alisisitiza Manara

Salaam… Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza. na naweza sema kitu, kwanza niwape pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mm c mtu ninayeamini uonevu c mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, c mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale panapopaswa kurekebishwa, na always ntabaki hvyo, Juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniarifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu jpili ya jana asubuhi, wakati huo nikiwa zbar kwa masuala yangu ya kifamilia, na ofisi ikaiandikia Tff barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi jnne ya kesho kwa kuwa ntakuwa nipo Dar. barua iliwafikia na bnafsi nikaongea na Afred lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yy na imegongwa muhuri na katibu mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hyo ni jioni ya Ijumaaa , Jmosi nikampigia Alfred kuulizia kikao hcho cha kamati kimepangwa lini,akanijibu jtatu ya leo atanijibu, jana tena mkasikia mliyosikia,ni uharaka upi ilionao tff wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa? natural justice nchi hii haitambuliki!!wahaini na wauaji nao pia husikilizwa,,iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake? kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu bnafsi barua ya Tff , hv ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar na sikuwa nimeiona na vp klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji? na hv Tff hawajui kuwa mm nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu? nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu? nimemuona kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka, hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaid kwa vwango vya mpira wetu, ila nawaambia Tff Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili, lakini nna moyo wa Simba, ntapambana kwa kiwango cha juu sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango, na ntaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa,nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki, na nawahakikishia kikao kitakachokaa

A post shared by Haji S Manara (@hajismanara) on

Leave a comment