Harmorappa Ampa Ushauri Rais MagufuliHarmorappa Ampa Ushauri Rais Magufuli

0
Msanii Harmorapa ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Kiboko ya mabishoo’ amefunguka na kutoa ushauri kwa Rais Magufuli juu ya mambo ambayo angependa kuona Rais anayafanyia kazi.
Harmorapa akiwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachofanyika kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano  ameshauri Rais Magufuli kuboresha zaidi miundombinu ambayo inaweza kuleta tija na maendeleo kwa nchi lakini pia amemuomba awaangalie pia wasanii ili waweze kunufaika na kazi zao.
“Rais Magufuli unajua yeye ndiye mwenye nchi sasa, hivyo mimi namuomba aboreshe zaidi suala la miundombinu natambua amefanya mambo mengi na makubwa kwenye sekta hiyo ila aboreshe zaidi, lakini pia namuomba Rais Magufuli aendelee kuwafinya wale wajanja wajanja kama ambavyo anafanya saizi na kingine atuangalie na sisi wasanii na kazi zetu” alisema Harmorapa
Mbali na hilo Harmorapa amegusia suala la yeye kuonekana ni mtu wa kiki amesema kuwa yeye si mtu wa kiki bali hizo kiki zinamfuata yeye.
Facebook Comments
Share.

About Author