Home Michezo HARRY KANE MAJANGA TENA HUENDA AKAWA NJE YA DIMBA KWA MUDA MREFU

HARRY KANE MAJANGA TENA HUENDA AKAWA NJE YA DIMBA KWA MUDA MREFU

74
0

Na Yego Sholla

Harry Kane ameumia katika kifundon chake cha mguu wa kulia na kuna wasiwasi kwamba huenda akawa nje ya dimba kwa kipindi kirefu , na imeripotiwa kwamba ameumia katika sehemu ile ile ambayo aliumia msimu uliopita na kukaa nje kwa muda mrefu.

Kane alitoka nje dakika ya 34 kwenye mechi ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Bournemouth baada ya kugongana na Golikipa wa Bournemouth Asmir Begovic.

Kocha Mauricio Pochettino alithibitisha kwamba mwandishi wa Sky Sports, Greg Whelan wakati wa mapumziko kwamba jeraha hilo ni la mguu wa kulia na sehemu ile ile aliyoumia msimu uliopita dhidi ya Sunderland.

Kane alikuwa nje ya dimba kati ya Septemba mpaka Novemba ya 2016 kutokana na jeraha hilo la kifundo cha mguu wa kulia  kabla ya wiki mbili na nusu zingine nje ya dimba kati ya Machi na April 2017.

Na baada ya mechi Pochettino alisema:

” Nina wasiwasi , mpaka kesho ( Leo Jumatatu ) , siwezi kusema kitu chochote mpaka baada ya vipimo.”

” Bila shaka nina wasiwasi kuhusu yeye, na kifundo cha mguu . Ni matumaini yetu isiwe jeraha kubwa na pigo kubwa kwake na timu kwa ujumla . Tunatumaini atapona haraka sana na kurejea dimbani.”