Home Michezo HII NDO ADHABU ALIYOPEWA MKUDE NA KOCHA MFARANSA, BAADA YA KUCHELEWA NDEGE

HII NDO ADHABU ALIYOPEWA MKUDE NA KOCHA MFARANSA, BAADA YA KUCHELEWA NDEGE

283
0

Moja kati ya maswali yaliyowatinga wanaSimba wengi jana ilikuwa ni baada ya Kikosi cha Simba kutoka kikiwa hakina jina la nahodha wao wa zamani Jonas Mkude.

Moja kati ya Vitu vilivyokuwa vikiwachanganya hususani kwenye mitandao ya Kijamii ni ile taarifa ya Mkude Kuchelewa ndege wengi wakiamini Mkude hakwenda lakini Ukweli uliothibitishwa ni kwamba Mkude alisafiri siku ileile aliyoachwa na Ndege ikimlazimu kusafiri na ndege ya Mchana wakati wenzake wakiwa waliondoka Asubuhi.

BENCHI LA UFUNDI CHANZO MKUDE KUTOCHEZA.

Taarifa za ndani kutoka Klabu ya Simba  zinadai kuwa makocha wa Simba Mfaransa Pierre na Masoud Djuma kwa Pamoja walichukizwa na Kitendo hiko cha Mkude kuchelewa Ndege wakitafsiri kama Ni Utovu wa Nidhamu hivyo wakaamua kumpiga Benchi hata kwenye wachezaji wa Akiba akikosekana.

” Benchi la Ufundi limefanya hivyo ili kuhakikisha kunakuwa na Nidhamu ndani ya Kikosi hiko cha Simba na kufanya timu kuwa moja na kutokuwa na Mchezaji ambaye atajiona ni mkubwa kuliko timu “

Kilieleza chanzo chetu.

Simba katika mchezo huo   iliishia kupata alama moja mara baada ya kutoka sare ya bao 2 kwa 2 na Mwadui Fc waliokuwa wanafanya kazi ya kuchomoa Magoli ya Simba yaliyofungwa na John Bocco na Emmanuel Okwi