Hii ndo rekodi mpya aliyoweka Walcot UEFA Champions League - The Choice

Hii ndo rekodi mpya aliyoweka Walcot UEFA Champions League

0

arsenal-4

Magoli mawili ya winger wa Arsenal Theo Walcott kwenye mchezo wa Kundi A michuano yha UEFA Champions League dhidi Basel yamemfanya atengeneze rekodi yake kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu.

arsenal

Nyota huyo wa England amefunga goli lake la kichwa kwa mara ya kwanza katika michuano ya hiyo ya Ulaya.

arsenal-1

Walcott amefunga magoli mawili kwa mara ya kwanza katika mechi moja ya UEFA tangu October 2007 alipofanya hivyo dhidi ya Slavia Prague.

Matokeo hayo yamewafanya vijana wa Wenger kuchza mechi nane bila kupoteza kwenye mashindano yote tangu walipochezea kipigo cha magoli 3 mbele ya Liverpool siku ya ufunguzi wa ligi ya England.

Ushindi wa Arsenal dhidi ya Basela ni ushindi wa kwanza msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya kutoka sare katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya PSG.

arsenal-2

Matokeo ya mechi zote za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa September 28

arsenal-3

 

Share.

About Author