Hiki Ndicho Alichokifanya Nuh Mziwanda Baada ya Mke Wake Kujifungua Mtoto wa Kike - The Choice

Hiki Ndicho Alichokifanya Nuh Mziwanda Baada ya Mke Wake Kujifungua Mtoto wa Kike

0
BAADA ya mkewe, Nawal kujifungua mtoto wa kike, Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ameamua kumzawadia wimbo ikiwa ni njia ya kumshukuru kwa kuwa ni mwanamke wa kipekee kwake kuliko aliowahi kutoka nao kabla hajaingia kwenye ndoa.
Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, Nuh alisema anajivunia kupata mtoto wa kike aliyempa jina la Anyagile japokuwa alitamani angepata wa kiume lakini hana budi kumpokea kwa furaha ndiyo maana ameamua kumzawadia mkewe wimbo unaokwenda kwa jina la Anameremeta.
“Namshukuru Mungu kwa kunipa mtoto Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata nikatoa wimbo huo ambao ni zawadi kwa mke wangu kwani ni mwanamke wa tofauti kwangu kwani kanizalia mtoto mzuri ambaye ndiye wa kwanza kwangu, nina furaha sana kwa kweli,” alisema Nuh Mziwanda.
Share.

About Author