Home Michezo Huku SIMBA pumzi ikianza kukata,naiyona YANGA ikijiandaa kubeba Ndoo tena.

Huku SIMBA pumzi ikianza kukata,naiyona YANGA ikijiandaa kubeba Ndoo tena.

188
0

Hakika mbio za kushindania Taji la ligi kuu kwa msimu wa 2017/2018 zimekuwa za kusisimua sana kutokana na Timu nyingi kujipanga haswa tofauti na kipindi cha nyuma .

Kuongezeka kwa Timu kama Singida United kumechangia kuongeza radha ya ushindani katika Ligi ya hapa.

Pia uwepo wa udhamini kwa baadhi ya Timu umesaidia kuongezea ushindani wa Ligi.

SIMBA

Ni timu iliyofanya usajiri mzuri sana na wa gharama kubwa sana tofauti na misimu mingine iliyopita kwa miaka minne,

Simba ilianza vizuri sana katika ligi huku washambuliaji Boco na Okwi wakiwa ni tegemeo kubwa katika chachu ya ushindi wao.Simba imeonekana ni Timu inayotegemea wachezaji baadhi ili kuweza pata ushindi na kama wachezaji hao hawapo basi huwa inapata ushindi kwa tabu sana na pengine kushindwa kabisa kupata ushindi.

Kuumia kwa bocco kumeonyesha pengo kubwa sana kwa Simba huku mbadala kama yeye akikosekana kuweza kuziba pengo.

Kuumia kwa Okwi pia ni tatizo kwa sababu inakuwa haina mbadala ambaye anaweza kufanya kazi kama anayofanya yeye.

Hivyo inakuwa ni changamoto sana kuwategemea wachezaji wawili tu.

Draw ya juzi dhidi ya Stand itawafanya simba waanze kucheza kwa Presha michezobuake ijayo.Hii inaweza kuwaletea madhara katika kugombania Taji la ligi kuu.

YANGA

NI TImu ambayo haikufanya usajiri mkubwa sana zaidi ya kumchukua Ajibu na Tshishimbi.

Tatizo walilokumbana nalo no Majeruhi zaidi ya kumi wote ni wale muhimu pia ukata wa fedha ulioikumba Timu kusababisha hata mishahara ikawa ngumu kupata kwa wakati.

Hii ilisababisha kuanza kutumika kwa wachezaji wa akiba.Lakini hadi sasa wameweza kupambana na kuwakaribia wapinzani wao ambao ni simba kwa ukaribu sana.

Hii kwao inakuwa kama ni marali na ukilinganisha na walipitoka.Ni timu ambayo haimtegemei mtu mmoja sana kwa sasa.Pia kuanza kurejea kwa wachezaji muhimu katika Timu kwa mda muhimu kama sasa hii inafanya Yanga kuwa na nguvu na morali zaidi ya Simba ambayo kwa sasa inacheza kwa Presha.

Dalili hizi zinaonyesha Yanga anaweza kumalizia ligi vizuri zaidi ya Simba