Huyu ndiye Aliyeingia na Bastola Uwanjani akitaka kumpiga risasi Refa baada ya kukataa goli - The Choice

Huyu ndiye Aliyeingia na Bastola Uwanjani akitaka kumpiga risasi Refa baada ya kukataa goli

0

ATHENS, UGIRIKI: Ligi kuu ya soka ya nchini humo imefungwa kwa muda usiojulikana kwa mujibu wa serikali.

Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya Rais wa timu ya PAOK, Ivan Savvidis ambaye ni moja ya watu tajiri nchini humo kuingia uwanjani na bastola kupinga kukataliwa kwa goli la timu yake

Naibu Waziri wa Utamaduni na Michezo, Georgios Vassiliadis alisema kuwa ligi hiyo haitaendelea mpaka kutakapowekwa misingi na sheria na taratibu zitakazokubaliwa na wote

Bwana Ivan Savvidis aliingia uwanjani mara mbili akitaka kumkabili mwamuzi wa mchezo huo, Giorgos Kominis. Kitendo hicho kilisababisha mchezo huo kusimama kwa takribani saa 2

5,925 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author