Home News ISAAC GAMBA, MTANGAZAJI MTANZANIA WA DEUTSCHE WELLE UJERUMANI AKUTWA AMEFARIKI BONN BAADA...

ISAAC GAMBA, MTANGAZAJI MTANZANIA WA DEUTSCHE WELLE UJERUMANI AKUTWA AMEFARIKI BONN BAADA YA SIKU KADHAA

1162
0

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MTANGAZAJI wa michezo na burudani wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Deutsche Welle ya Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba ‘Mwanangu’ (pichani kushoto) amefariki dunia mjini Bonn nchini humo.
Habari za kuaminika kutoka nchini Ujerumani, zimesema kwamba Gamba alifikwa na umauti mapema wiki hili, lakini leo ndiyo imegundulika.
Hiyo ni baada ya Gamba kutoonekana ofisini kwake, Deutsche Welle mjini Bonn tangu Jumatatu jambo ambalo liliwafanya wafanyakazi wenzake waende nyumbani kwake na Polisi kumfuatilia na ndipo walipogundua amefariki baada ya kuvunja mlango.
Gamba ambaye ni miongoni mwa watangazaji waliowahi kujipatia umaarufu nchini Tanzania, amewahi kufanya kazi katika vituo kadhaa vya Redio kikiwemo cha Radio One Stereo, Radio Free Africa na Uhuru FM.
Mungu ampumzishe kwa amani Gamba. Amin.