Home Michezo ISHU YA SIMBA KUMNYEMELEA CHIRWA, YANGA WASEMA HAYA

ISHU YA SIMBA KUMNYEMELEA CHIRWA, YANGA WASEMA HAYA

31
0

ISHU YA SIMBA KUMNYEMELEA CHIRWA, YANGA WASEMA HAYA

Baada ya kuwepo taarifa za chini chini ambazo siyo rasmi kuwa Bilionea Mohammed Dewji Mo huenda akamwaga pesa ili kumnasa Straika wa Yanga Obrey Chirwa uongozi wa Yanga nao umejibu mapigo kwa kusema hawawezi kumwachia Kirahisi hivyo Chirwa aende kwa wapinzani wao Simba.

Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga   amesema licha ya kuwa yeye si msemaji wa masuala ya Usajili lakini hawezi kukubali kumwachia Straika Huyo na hata kamati ya Usajili inayoongozwa na Hussein  Nyika haamini kama inaweza kukubali kirahisi Kumuachia Obrey Chirwa.

” Mimi si msemaji sana wa masula ya usajili kwani sekta hiyo inaongozwa na Hussein Nyika (Ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Usajili Yanga) lakini navyojua mimi halitakuwa jambo rahisi kumwachia Obrey Chirwa. “

Wakati wa dirisha Kubwa la Usajili Simba walifanikiwa kuinasa saini ya kipenzi cha washabiki wa Yanga Haruna Niyonzima mara baada ya mchezaji huyo kumaliza mkataba ndani ya Yanga na Kushindwa kufikia makubaliano ya Kuongeza mkataba  mwingine ndani ya Klabu hiyo ya Yanga.

Huku Yanga nao wakilipiza Kimya Kimya na Kumsajili mchezaji Ibrahim Ajib kutoka Simba ambaye naye washabiki wa Simba wengi waliumia kwa fundi wa Kuchezea Mpira kutua kwa wapinzani wao Yanga.