Home Michezo Ishu ya Simba kununua Mkataba wa Chirwa Yanga hii hapa

Ishu ya Simba kununua Mkataba wa Chirwa Yanga hii hapa

63
0

Ishu ya Simba kununua Mkataba wa Chirwa Yanga hii hapa

Kizuri kinajiuza na Kibaya Kinajitembeza ndiyo kauli unayoweza ukaitumia kwa Mchezaji Obrey Chirwa, siku za Karibuni amekuwa Gumzo kutokana na Pata kosa zake kwenye penati lakini ni wazi anapokuwa uwanjani shughuli yake wapinzani huwa wanaiona.

Kuna taarifa za Uhakika kuwa Simba wameanza kumnyemelea mchezaji Obrey Chirwa kwaajili ya msimu Ujao hivyo viongozi wa Usajili  wamekuwa wakifanya naye mazungumzo ili kumalizana naye.

Chirwa  amebakiza Miezi minne Yanga na Inaelezwa Kaimu mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba Kassim Dewji amekuwa akiwasiliana Naye akimwambia Kuwa wao kama Simba wako tayari kumlipa hata fedha ya Miezi hiyo Minne iliyobaki Yanga.

Na kuwasiliana huko kati ya Simba na Chirwa ndiyo sababu ya Mchezaji huyo kukataa kuongeza mkataba kwa Chirwa kila anapofatwa na Viongozi wa Yanga kwaajili ya Kuongeza Mkataba.

DEWJI AKATAA KUWASILIANA NA CHIRWA

Hata hivyo anayetajwa sana kuwasiliana na Chirwa Kassim Dewji amekana kuwasiliana na Mchezaji huyo anayeongoza kwa Magoli katika Klabu Yake ya Yanga Ligi Kuu VPL akiwa na Magoli 10.

Dewji pia amesema Bado kikosi cha Simba kinahitaji wachezaji kadhaa wenye uwezo na Uzoefu wa Michuano ya Kimataifa ili kuzidi kukiimarisha kikosi cha Simba ambacho msimu huu kimekuwa Mcharo.