Home News JPM: Mimi ni Jiwe Kweli Kweli, Sitishwi Wala Sitishiki

JPM: Mimi ni Jiwe Kweli Kweli, Sitishwi Wala Sitishiki

36
0

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema uwepo wake madarakani ni kutaka kuwatoa Watanzania katika shida mbalimbali walizokuwa nazo na kuwapelekea hali amayo wataishi kwa raha ili siku atakapokuja kufa basi hata Mungu ampe nafasi ya kuwaongoza Malaika mbinguni.

Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Singida wakati wa kuzindua kiwanda cha mafuta ya Alizeti, Mount Meru Millers kilichojengwa mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John P. Magufuli akiombewa na viongozi wa Kidini kutoka Singida mara baada ya kufungua kiwanda cha usindikaji wa Alizeti hii leo – Machi 11, 2018,

“Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa mna Rais kweli kweli, jiwe kweli kweli. Sitishwi wala sitishiki, mimi jukumu langu ni kuhakikisha nawavusha Watanzania kutoka kwenye shida na kwenda mahali kwenye raha.

 

 “Ninajua hiyo ndio itakuwa sadaka yangu kwa Watanzania ili kusudi hata siku moja nikienda huko mbinguni, kutokana na mimi kuwa kiongozi mzuri, Mungu atakaponihitaji akanichague niweze kuongoza Malaika polepole kwa sababu ninajua kuna maisha mengine baada ya maisha ya hapa duniani”, amesema Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais amewaomba sana viongozi wa dini, masheikh na wale watu mbalimbali katika imani zao tukuitanguliza Tanzania kwanza, huku akiwataka wasitumike. Amewataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikomboa na kujiongezea kipato cha maisha.