Juma Abdul atajwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa 2015/2016, orodha kamili ya washindi ipo hapa - The Choice

Juma Abdul atajwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa 2015/2016, orodha kamili ya washindi ipo hapa

0

JUMAHitimisho ligi ya msimu wa 2015/2016 imekamilika kwa utolewaji wa zawadi kwa washindi wa kombe la msimu wa 2015/2016 ulioambatana na utoaji wa tuzo kwa vipengele mbalimbali.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba amemtaja mchezaji bora wa msimu kuwa ni Juma Abdul wa Yanga ambaye amewashinda wenzake ambao ni Mohammed Hussein na Chiza Kichuya.

Juma Abdul kwa msimu umeomalizika amecheza michezo 25, dakika 2,069 na kufanikiwa kufunga magoli 3 huku akipewa kadi moja ya njano.

Orodha kamili ni;
Mchezaji Bora wa Msimu – Juma Abdul – Milioni 9.2

Mchezaji Bora Chipukizi – Mohammed Hussein – Milioni 4

Mchezaji Bora wa Kigeni – Thaban Kamusoko – Milioni 5.7

Goli Bora la Msimu – Ibrahim Ajib – Milioni 3

Golikipa Bora wa Msimu – Aishi Manula – Milioni 5.9

Kocha Bora wa Msimu – Hans Van Der Pruijm – Milioni 8

Refa Bora wa Msimu – Ngole Mwangole

Timu Yenye Nidhamu – Mtibwa Sugar – Milioni 17.2

Mfungaji Bora Msimu wa 2015/2016 – Amissi Tambwe – Milioni 5.7

Washindi wa msimu;
4. Prisons – Milioni 21
3. Simba – Milioni 29
2. Azam – Milioni 42
1. Yanga – Milioni 81

Share.

About Author