Home News KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WIZARA YA MADINI

KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WIZARA YA MADINI

1377
0

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo imekutana na Wizara ya Madini kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Wizara hiyo  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini Ndugu Augustine Ollal akiwasilisha taarifa ya Wizara hiyo  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 katika kikao cha Kamati ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Oofisi za Bunge Jijini Dodoma. Wengine ni manaibu Mawaziri wa Wizara hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo (katikakati) na Mhe. Doto Biteko.