KAULI YA JERRY MURO KUHUSU MANJI KUKODISHIWA TIMU YA YANGA - The Choice

KAULI YA JERRY MURO KUHUSU MANJI KUKODISHIWA TIMU YA YANGA

0

Msemaji wa Yanga Jerry Muro
Ndugu zangu kabla ya kuanza kutoa comment napenda sana tujue historia ya uendeshaji wa club na mpaka hapa club ilipofika kisha ndio tuje kwenye hoja ya msingi.
Kwa kifupi club imekuwa haitengenezi faida katika uendeshaji na hii inatokana na mfumo ulioasisiwa miaka ya nyuma ya uendeshaji wa club.
Tumekuwa na wanachama na mashabiki ambao kwa kiasi kikubwa hawajaweza kuisaidia timu katika uendeshaji. Club kwa muda wa miaka 4 imetegemea nguvu ya upande mmoja wa Mwenyekiti katika kulipa mishahara na kujiendesha.
Unaweza kuuliza kwa nini mtu mmoja, hili ni suala mtambuka sana kwa sababu hakuna makampuni yanayotaka kuwekeza kwenye soka la ubabaishaji hakuna mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji na hata hawa wachache wanaowekeza mikataba yao ni ya kinyonyaji sana.
Kutokana na sababu hizo chache na pressure za mashabiki kutaka matokeo mazuri bila kuangalia miundombinu mingine ya kuwezesha matokeo mazuri mfano uwekezaji wanachama wamekuwa wanataka matokeo mazuri jambo linalosababisha mtu mmoja aliyeko madarakani kutumia nguvu kubwa kupata ushindi na hapa ndipo tulipofika sasa.
Nirudi kwenye hoja ya msingi, kutokana na uhitaji wa timu kutaka kufanya vizuri pasipo kuwepo na mipango mizuri ya muda mrefu ambayo inasabishwa na aina ya upatikanaji wa viongozi imefanya kila kiongozi anaeingia madarakani aingie na mipango ya muda mfupi tu maanayake uhakika wa kukaa madarakani unakuwa mdogo kutokana na pressure za wanachama.
Sasa Manji kaamua kuja na mfumo ambao kwanza utamuwezeshaji kuja na mipango ya muda mrefu yenye uhakika wa kutekelezwa kutokana na kulindwa na makubaliano hivyo kama ni kuwekeza atawekeza vizuri kwa kuwa anajua yuko assured na fedha atakazoweka.
Hii itasaidia Yanga kwanza kupata matokeo mazuri ya uwanjani lakini pia kuwa na uwekezaji endelevu mfano kwenye bidhaa za Yanga ambazo zinauzwa bila club kunufaika lakini pia ameondoa mzigo mkubwa wa madeni ya Yanga ambayo yalikuwa yanaikumba timu mfano gharama za mishahara kambi vitendea kazi hivyo vita kuwa juu ya Manji na kubwa ni kuwa Yanga ikianza kutengeneza faidi itakuwa inapata asilimia 25 ya faida na inapotokea hasara anabeba Manji mwenyewe.
Kwa maoni yangu mimi Jerry Muro nadhani kwa sasa ni hatua nzuri ya kuanza najua kuna changamoto zitajitokeza lakini lazima tukubali kuanza mahali kwanza kisha twende mbele mana hakuna modal nyingine nzuri ambayo imejitokeza kwa sasa zaidi ya ile ya Simba ya uwekezaji na hii yetu ukiangalia kwa jicho la ndani zaidi uwekezaji wa Mo na hii ya Manji hauna tofauti kubwa sana sema huu wa kwetu tunabaki na asset zetu wenyewe na club yetu wenyewe tofauti na wale wenzetu ambao wanatoa mpaka rasilimali zao.
Sisi tunaweza pia kuwekeza kwenye majengo yetu na asset zetu nje ya mkataba wa Manji mana yeye anataka timu management na brand management na sio club assets, tukitazama mifumo ya uendeshaji wa vilabu vikubwa vya Ulaya ni kama huu wa Manji maanayake utaona mwarabu katoka Uarabuni kaenda England kachukua Manchester City yeye hajachukua majengo wala assets kachukua management tu na brand ya Man City.
 
TUTAFAKARI KWA KINA NA KAMA TUNA MAWAZO MBADALA TUYATOE NA SIYO KUPINGA BILA KUTOA SULUHISHO KAMA HUU NI MBAYA TUENDE NA MFUMO GANI?
 
Ni mawazo yangu mimi binafsi niko tayari kukosolewa na kupingwa kwa hoja.
 
Jerry Cornel Muro
Facebook Comments
Share.

About Author