Home Burudani Kauli ya Mzee wa Upako Kumchukia Ali Kiba sababu ana Kiburi

Kauli ya Mzee wa Upako Kumchukia Ali Kiba sababu ana Kiburi

93
0

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), #AnthLusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako, amemtaja msanii ambaye anamkubali kati ya Alikiba na Diamond pamoja na kutoa sababu zake.
_
Akiongea na kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM, Mzee huyo wa Upako amesema anampenda sana #Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu lakini #Alikiba ni kiburi.
_
👉“Mimi nampenda sana Diamond kwa sababu ni mnyenyekevu, Simpendi Alikiba kwa sababu ana kiburi, nadhani kwa sababu amekaa Kariakoo,” amesema #Lusekelo.
_
Mchungaji huyo ameongeza kwa kusema,👉 “Ukipigia simu Diamond anapokea kwa unyenyekevu ila Alikiba anapokea kwa maringo. Ndio maana Diamond amefika mbali.”
TOA MAONI YAKO HAPA