KIIZA ATUMBULIWA JIPU SIMBA - The Choice

KIIZA ATUMBULIWA JIPU SIMBA

0

Taratiibu mambo yanaanza kutimia baada ya uongozi wa benchi la ufundi la Simba, “kumchinjia baharini” mshambuliaji wao Hamisi Kiiza raia wa Uganda kwa tuhuma za utukutu au utovu wa nidhamu.

Si Kiiza tu, Waganda wenzake pia Juuko Murshid na Brian Majwega pamoja na Mkenya Paul Kiongera na Mrundi Emery Nimubona waligomea safari ya kwenda Songea kucheza mchezo huo kwa shinikizo la kulipwa kwanza mshahara wao ambao zilikuwa zimepita siku tisa tu.

Mbali na kuukosa mchezo huo, pia waliukosa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar wikiendi iliyopita ambao Simba ilishinda bao 1-0 ugenini lililofungwa na Abdi Banda.

Facebook Comments
Share.

About Author