Home News KIKAO KAZI CHA 15 CHA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO, UHUSIANO NA ITIFAKI...

KIKAO KAZI CHA 15 CHA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO, UHUSIANO NA ITIFAKI SERIKALINI

1138
0

DAR ES SALAAM, JUMANNE, 12 FEBRUARI, 2019

Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo,  kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo na Chama cha Maafisa Habari Serikalini (TAGCO) wameandaa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi, na Wakala wa Serikali (MDAs) kitakachofanyika Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 18– 22 Machi 2018.

Kikao kazi hiki kinachotarajiwa kuhudhuriwa na jumla ya Maofisa 300 ni cha 15 katika mfululizo wa vikao vinayofanyika kila mwaka kwa lengo la kuwajengea Washiriki uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za Serikali. Aidha, kikao kazi hulenga pia kuziimarisha Idara/Vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano Serikalini ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

 

Pia, Kikao Kazi, kinatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 18 Machi 2019 na kufungwa rasmi tarehe 22 Machi 2019 na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb).

 

Aidha, katika Kikao Kazi cha 15, jumla ya mada 10 zitawasilishwa. Mada hizo zinalenga kujenga uwezo wa Maafisa kwenye masuala mbalimbali yahusuyo habari, mawasiliano, uhusiano na itifaki.

 

Mada hizo zitawasilishwa na Wataalam watakaoleta uzoefu mpana katika mawasiliano. Pia, Kikao kazi kitatoa fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya Maafisa Mawasiliano na wadau wengine wa habari.

 

Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wanahimizwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 10 Machi, 2019.

 

TAGCO ni chama kinachowaunganisha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano walioko Serikalini.

 

Mkutano huu wa Maafisa Habari kwa mwaka huu, umedhaminiwa na: TANAPA, NCAA,  TANESCO, SHELL, SSRA, PSPTB,  na BOT.

 

 

Imetolewa Na:

SARAH KIBONDE MSIKA

Makamu Mwenyekiti

TAGCO