Home Michezo Kinachosubiriwa Kuthibitisha kama Niyonzima Kasaini Yanga au Simba

Kinachosubiriwa Kuthibitisha kama Niyonzima Kasaini Yanga au Simba

17
0

Image result for haruna niyonzima
Kinachosubiriwa Kuthibitisha kama Niyonzima Kasaini Yanga au Simba

Ndugu msomaji wa MsindiForums Kukiwa na Taarifa Nyingi kuhusu UTATA juu ya Usajili wa Niyonzima, Wengine wakiamini kasaini Simba wengine wakiamini ataendelea Kubaki Yanga.

Vyombo vingi vya habari vimeandika habari ya Niyonzima katika Namna ya kuwaacha Wapenzi na washabiki wa Vilabu hivi vikubwa kubaki na majibu yasiyojitosheleza.

KAMA NIYONZIMA ATASAINI YANGA
Kama Niyonzima Itakuwa kasaini Yanga basi itajulikana mapema sana kwani Bado wanamkataba naye kwahiyo hakutakuwa na Chakuficha, Hivyo watu wataona hata zile Picha za Mazungumzo na Kipindi anasaini zitakuwa Rahisi Kuonekana.


KAMA ATASAINI SIMBA
Itakuwa kama Yanga wanavyoficha kwa Ibrahim Ajib na Itabidi washabiki wa Simba wasubiri mpaka Mkataba wa Niyo uishe Yanga, Akisaini Simba tusitegemee Kuona hata Picha akisaini kwa wakati huu kwani inaweza kuwagharimu Simba kama Ilivyokuwa kwa Yanga wakati walipomsaini Ramadhan Kessy.