Home Michezo Kocha Simba apagawa na Mchezaji wa Asante Kotoko azungumzia Kumsajili

Kocha Simba apagawa na Mchezaji wa Asante Kotoko azungumzia Kumsajili

192
0

Kocha Simba apagawa na Mchezaji wa Asante Kotoko azungumzia Kumsajili

Hakika siku ya Jumatano 8.8.2018 ilikuwa moja kati ya Siku bora zaidi
kwa Simba kwa Mwaka huu kwani licha ya Kufanya mambo mengi kama Klabu
ikiwemo kutambulisha Timu zao za Vijana na ile ya wanawake na timu kubwa
Ya Simba walipata nafasi ya Kucheza na Moja ya Timu bora kabisa barani
Afrika.

Katika mechi hiyo ilishuhudiwa Simba ikimaliza mchezo kwa kubanwa kwa sare ya bao 1 kwa 1 bao la Simba likifungwa na Emmanuel Okwi.

KOCHA APAGAWA NA RASTA WA ASANTE KOTOKO.

Wakati watu wengi walioshuhudia mechi hiyo wakipagawa na uwezo wa
Rasta wa Asante Kotoko kumbe hata kocha wa Simba Patrick Aussems naye
alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wakivutiwa naye kutokana na
Kuichachafya Vilivyo safu ya Ulinzi ya Simba.

Mchezaji mwenyewe ambaye wengi walimkariri kutokana na RASTA zake
anaitwa Yacouba Songne ambaye licha ya Kucheza Asante Kotoko ya Ghana
lakini ni raia wa Burkinafaso.

Kocha wa Simba Patrick Aussems raia wa Ubelgiji akizungumza baada ya
Mchezo huo ameweka wazi kuvutiwa kwake na STRAIKA huyo na kusema kuwa
kama atahitaji straika wakati wa dirisha dogo basi chaguo lake la kwanza
litakuwa ni mchezaji huyo Yacouba Songne kutoka Asante Kotoko wazee wa
Kumasi.