Home Michezo KOCHA WA SIMBA, APATA DILI JIPYA COASTAL

KOCHA WA SIMBA, APATA DILI JIPYA COASTAL

1755
0
KOCHA WA SIMBA, APATA DILI JIPYA COASTAL
KOCHA WA SIMBA, APATA DILI JIPYA COASTAL

COASTAL Union nao wameanza jeuri ya fedha baada ya kuweka mipango kabambe ya kumngíoa Kocha Mkuu wa zamani wa Simba, Darln Kerry, kutoka kikosi cha Gor Mahia ya Kenya, ambao ni mabingwa nchini humo.

Taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho zinadai kuwa, wanataka kumvuta Kerry ili kuhakikisha msimu huu wanakuwa tishio kama ilivyo kwa Gor Mahia, ambao hawashikiki Ligi Kuu nchini Kenya.

Taarifa hizo za Kerry zimezagaa mpaka kwenye vijiwe mbalimbali vya soka Jijini Tanga, ambako wadau wa soka wanaeleza kwamba dili hilo likifanikiwa timu yao itakuwa moto wa kuotea mbali.

Coastal Union, ambayo imepanda daraja msimu uliopita, imecheza michezo mitatu, imeshinda mmoja na kutoka sare miwili na inatajwa kuwa kama Kerry akija kikosi hicho kitafumuliwa na kujengwa upya, ili kiwe na makali zaidi.

Kufuatia tetesi hizo, Dimba lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, Hemed Aurora, ambaye alisema bado wanamtambua Juma Mgunda kama kocha wao mkuu na hizo taarifa ni za kumpunguzia morali.

ìSisi tunaye Juma Mgunda, hilo la Kerry nasikia kutoka kwako, nadhani tusilipe nafasi, kwani linaweza kutufanya kushindwa kuwekeza kwenye mechi zetu,î alisema.

Alisema mpaka sasa hawajafikiria kutafuta kocha mwingine, kwani aliyepo anatosha na tokea ligi hiyo ianze hajafanya vibaya kwenye michezo

Leave a comment