Home Michezo KRC Genk Inayochezewa na Mbwana Samatta Inaungana na Man United 16 Bora...

KRC Genk Inayochezewa na Mbwana Samatta Inaungana na Man United 16 Bora ya Europa League

32
0

Usiku wa February 23 2017 mtanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji aliingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Europa League kwa kuitoa FC Astra ya Romania.

Samatta akiwa na KRC Genk waliikaribisha FC Astra ya Romania katika mchezo wao wa pili wa marudiano wa Europa League, katika uwanja wa Luminus Arena ikiwa ni wiki moja imepita toka watoke sare ya 2-2 ugenini.

Katika game hiyo ya marudiano iliyochezwa na KRC Genk kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Pozuelo kwa faulo dakika ya 67, wameiondoa FC Astra kwa jumla ya goli 3-2, hivyo Genk wanaungana na timu nyingine 15 kucheza hatua 16 bora ya Europa League ikiwemo Man United.