Home Michezo Kuelekea fainali ya Simba vs Mbao FC, TFF wajikanyaga

Kuelekea fainali ya Simba vs Mbao FC, TFF wajikanyaga

163
0

Kuelekea fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Klabu ya Simba na Mbao FC, shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) bado limeendelea kushikwa na kigugumizi ni uwanja upi utakaotumiwa kucheza mechi hiyo ya fainali.

TFF, kabla ya michuano hiyo kuanza msimu huu, hawakutangaza ni uwanja gani utatumiwa kwa ajili ya Fainali hiyo, kitu ambacho hata wenyewe wameshindwa kuelezea na badala yake kupanga kuchezesha Droo ya kujua ni uwanja gani utatumiwa kwa ajili hiyo.

“Ni kweli bado haijajulikana ni uwanja gani utatumika lakini leo au kesho tutachezesha Draw ambayo itaamua ni uwanja gani utakaotumiwa kati ya CCM Kirumba wa Mwanza na Uwanja wa Taifa“Alisema Alfred Lucas Ofisa mawasiliano wa TFF kwenye mahojiano yake na EFM.

Hata hivyo, Baada ya ushindi wa Mbao FC wa goli 1-0 dhidi ya Yanga wikiendi iliyopita, Rais wa TFF,Jamal Malinzi aliandamwa mitandaoni na wadau wa Soka wakitaka kujua ni uwanja gani utatumiwa kwa ajili ya michuano, kilichompelekea kutoa mwongozo kwa kutweet “Draw ya host venue wa final ya Federation Cup itafanyika live @azamtvtz katika tarehe na muda utakaopangwa.Fainali ni tar 28/05 #fairplay”

Leave a comment