Home News KUTEKWA KWA ‘MO’ VYAMA VYA UPINZANI VYATAKIWA KUTOICHAFUA SERIKALI

KUTEKWA KWA ‘MO’ VYAMA VYA UPINZANI VYATAKIWA KUTOICHAFUA SERIKALI

1459
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWANAHARAKATI, Mpambanaji huru na Mzalendo Cyprian Musiba, amevitaka vyama vya Upinzani kuacha kutumia fursa ya kutekwa kwa mfanyabiashara na mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji kuichafua serikali.

 

Mwanaharakati, Mpambanaji huru na Mzalendo Cyprian Musiba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Bilionea huyo,anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri alipokuwa akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2018.
Kauli hiyo ya Musiba imekuja siku moja baada ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani mbunge wa Jimbo la Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema kuitaka Serikali kuomba msaada kwa vyombo vya kimataifa kuja kufanya uchunguzi huru juu la vitendo vya utekaji vinavyoendelea nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Musiba amesema hayo aliyozungumza jana Lema ni maazimio ya kikao kilichofanyika usiku wa Oktoba 15, 2018 ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yenye mkakati wa kuichafua serikali kwa kuihusisha na vitendo hivyo.
“Nishasema kwamba kwa mtu yeyote anayemshambulia rais nitajitokeza kusema kwa sababu mimi ni mfuasi kweli kweli wa rais na nipo tayari kupambana nao kwa kila namna,” alisema Musiba.
Musiba amedai kuwa baada ya mkutano wa Lema jana usiku viongozi wa Chadema pamoja na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe kwa ajili ya kujipongeza na kufurahia kutekwa kwa ‘MO’kutokana na kwamba suala hilo linaichafua serikali.
Alimtaka Lema kutambua kuwa Rais ana mambo mengi yakufanya hivyo si lazima atoe matamko kwani tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola linatosha.
Aidha amelishauli Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa mlinzi wa mwenyekiti wa Chadema aliyamtaja kwa jina moja la Singo, kupotea kwa Ben Saanane pamoja na kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.