Home Michezo Kwa maamuzi haya ya Mbelgiji siku za Masoud Djuma zinahesabika

Kwa maamuzi haya ya Mbelgiji siku za Masoud Djuma zinahesabika

1676
0

Kwa maamuzi haya ya Mbelgiji siku za Masoud Djuma zinahesabika

Simba leo inakwea pipa kuelekea Mkoani Mtwara kwaajili ya mchezo kati yao dhidi ya Ndanda ya mkoani humo mechi itakayochezwa Jumamosi 14 September katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Lakini kuelekea mchezo huo dalili za Kocha Masoud Djuma kupigwa chini zimeanza kuonekana kutokana na maamuzi ambayo bosi wake Kocha Patrick Aussems ameyachukua kuelekea safari hiyo ya Mtwara.

Aussems amewaambia viongozi wa Simba kuwa kocha wake msaidizi Masoud Djuma asiongozane na Kikosi cha Simba na badala yake abakie na wachezaji watakaobakia Dar Es Salaam awasimamie katika mazoezi wakiungana na kikosi cha timu B.

Kocha Patrick AussemsĀ  ametetea maamuzi yake kwa kusema kuwa huo ni Utaratibu wake wa kila sehemu anayofanya kazi lengo likiwa ni kuhakikisha wachezaji wanaosalia Dar wanakuwa fiti

Siku chache zilizopita Iliandikwa na baadhi ya Vyombo vya habari kuwa Kocha Masoud Djuma yuko mbioni kupigwa chini ndani ya Simba na kwa dalili hizi imeanza kuthibitika

Leave a comment