Mama Ashura Apasua Jipu Adai Maneja wa Timamu TV ni Mume Wake

0
mama ASHURA

Muigizaji wa Timamu Entertement, Mama Ashura amepinga vikali tetesi zilizozagaa kuwa amesababisha kuondoka kwa muigizaji Mkali Wenu katika kampuni ya Timamu kwa kuwa anamahusiano yasio rasmi na bosi wa kampuni hiyo.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyu ambaye ni mahiri awapo katika kazi yake amedai hatembei na Meneja wake bali Meneja wake ni mume kabasa wa ndoa.

“Watu wanashindwa kuelewa mimi sitoki na meneja wangu, meneja wangu ni mume angu kabisa, watu wanatakiwa wajue, nina miaka naye sita kabla watu hawajanijua kama Mama Ashura na nina mtoto naye kwa hiyo familia zetu zinajua kabisa huyu ni mke na mume,” amesema Mama Ashura.

Alisisitiza kuwa “Baada ya watu kuona nimetoka kama Mama Ashura mwaka juzi, wakati mimi nipo muda mrefu kwa hiyo watu wasinichukulie mimi namna gani, watu wasinichukulie kisa natoka na fulani ndiyo maana amepewa nafsi hapana, mimi nimeanza sanaa kabla sijamjua Timos ,Mume wangu.”

Facebook Comments
Share.

About Author