Home Mahusiano MAMBO 10 YAKUZINGATIA KABLA YA NDOA.

MAMBO 10 YAKUZINGATIA KABLA YA NDOA.

386
0

1. Jifunze kuwa mkomavu sio kudeka deka kwa vitu vidogo unataka mpaka wazazi wakufanyie. Mfano kuna baadhi ya vijana ni “MIJEBA” lakini bado wanaomba pesa za kunyolea ndevu kutoka kwa wazazi wao halafu unataka kuwa mume..
2. Jitahidi kuhudhuria mafunzo mbalimbali juu ya mambo ya ndoa kabla ya ndoa pre-marital trainings/seminars.
3. Soma vitabu mbalimbali vya mambo yanayohusu ndoa ama namna ya kuingia kwenye ndoa.
4. Sikiliza vipindi vya vyombo vya habari vinavyofundisha mambo yanayohusu ndoa ama namna ya kuingia kwenye ndoa.
5. Epuka misimamo migumu na isiyo ya msingi ya kimila au kimakabila zingatia nyakati na utakatifu.

Soma: Mazingira Ambayo Yanaweza Kuchochea Usaliti Kwa Wanandoa.


6. Jifunze mambo Mema, uyafuate na usitafute mifano ya walioshindwa katika ndoa zao kama nguzo ya kuegemea.
7. Tafuta kujua Baba mzuri anakuwaje au mama mzuri anakuwaje.
8. Anza kujifunza sifa juu ya mume mzuri yukoje na Mke mzuri yukoje.
9. Jifanyie Maboresho wewe Mwenyewe yaani Improve yourself.
10. Rudisha Tabia njema za zamani ulizoziacha. – Mch. Peter Mitimingi.

By Chief Hope