Home Mahusiano Mambo 9 ya kuzingatia unapokwenda kuonana na mpenzi wako kwa mara ya...

Mambo 9 ya kuzingatia unapokwenda kuonana na mpenzi wako kwa mara ya kwanza

498
0

MAHUSIANO

Unapokwenda kuonana na mpenzi wako kwa mara ya kwanza, namna utakavyokuwa ukionekana, inamaana kubwa sana. Ukweli ni kuwa muonekanao wako, namna ulivyovaa unaweza kuamu kama utapewa nafasi ya ‘second date’, hivyo vaa vizuri na pendeza.

Kama unakwenda kwenye ‘date’ alafu uko rafu rafu tu, hii inatoa ujumbe kwa mwenza wako kuwa humjali na kuwa vyovyote utakavyovaa kwako wewe ni sawa.

Basi, ni namna gani ya mwanaume unaweza na ukapendeza unapokwenda kuonana na mpenzi wako mara ya kwanza?

1. Usivae nguo za kukubana sana

skinny-jeans

Ukivaa suruali inayokubana itakunyima kukaa kwa uhuru, mara uipandishe, huwezi kupiga hatua vizuri, mwisho wa siku unaweza kujikuta umeharibu usiku wako na mpenzi wako kwa sababu ya nguo inayokufanya usiwe huru

2. Kuwa mtanashati

Hakikisha kama umevaa shati umelipasi limenyooka vizuri, nywele umechana sawia, kucha umekata vizuri, hili litamfanya mpenzi wako akuona namna ulivyo ‘smart’ na muajibikaji.

3. Usithubutu kuvaa mtindo ambao hujawahi kuuva kabla

Unapotaka kutoka, usivae mtindo mpya wa nguo, kuwa halisi, kuwa wewe, vaa kama unavyovaa mara zote. Kumbuka kuwa jinsi unavyovaa huelezea wewe ni mtu wa aina gani, na kama sio kawaida yako kuvaa mtindo huo uliouchagua atagundua tu.

4. Usiweke vikorombwezo vikazidi

2-chainz-rapper

Watoto wa mjini wanasema ‘keep it simple’, huna haja ya kuvaa michezi, mipete, misaa kibao uanze kuwa kama mwanamuziki wa Marekani. Ukivaa saa moja tu mkononi inatosha.

5. Usivae nguo zenye maandishi

witty

Kuvaa nguo zenye maandishi kwenye ‘date’ kwa mara ya kwanza kuna hatari mbili, moja utaonekana kuwa haupo ‘serious’ kutokana na ujumbe uliopo kwenye nguo yako lakini pili, ujumbe unaweza kumkera mwenzako.

6. Marashi

lady

Kujiweka smart unahitaji na marashi ili unukie mwanana, lakini sasa yasizidi kiasi kwamba ukifika mahali kila mtu anafunika pua sababu unawasababishia mafua. Hii itafanya usiku wako kuwa mbaya, jipulizie marashi ila kwa kiasi.

8. Rangi ya nguo

Chagua rangi ya nguo ambayo itavutia na pia itakayoendana na mazingira, sio unavaa nguo inang’aa kama ‘reflector’ ya gari.

9. Usivae miwani au kofia ambazo zitakufunika uso kiasi kwamba mtu akitaka kukuona usoni hadi ainame chini.