MAN CITY YAPIGWA UEFA: SASA FAINALI NI MADRID DERBY, ATLETICO VS REAL MADRID - The Choice

MAN CITY YAPIGWA UEFA: SASA FAINALI NI MADRID DERBY, ATLETICO VS REAL MADRID

0

Baale-UEFA

Manchester City imeshindwa kufika fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kufurukuta kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya mabingwa mara 10 wa taji hilo Real Madrid.

Baada ya sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza, Real walipata goli lao pekee lililowapa ushindi kufuatia krosi ya Gareth Bale kumgonga Fernanho kisha kujaa wavuni.

Shuti la Fernandihno liligonga lakini Real ilitawala mchezo wao walipata nafasi kupitia kwa kiungo Luka Modriclakini shuti lake liliokolewa na Joe Hart.

Ushindi huo unaifanya Real Madrid ikutane na Atletico kwenye michuano ya Ulaya.

Kwahiyo, Real Madrid itakuta na kikosi cha Luis itacheza fainali dhidi ya Atletico Madrid kwenye dimba la San Siro May 28, 2016

Facebook Comments
Share.

About Author